Cheche Za Kiswahili Grade 1

KSh 250.00

Description

Smart Beginners Cheche za Kiswahili Kitabu Cha Mwanafunzi Gredi ya 1 kimeandikwa kwa kuzingatia yaliyomo kwenye ruwaza ya Mtaala wa Kiumilisi (CBC) ili kumfaa mwanafunzi kutekeleza shughuli mbalimbali za ujifunzaji. Shughuli zilizopendekezwa katika kitabu hiki zitamwezesha mwanafunzi kuwa na umilisi wa stadi mbalimbali. Sifa zake kuu: Vipengele vyote vya mada mbalimbali kwa mujibu wa mtaala mpya. Picha na michoro angavu kwa ajili ya kumwezesha mwanafunzi kuelewa matini. Shughuli tagusani kuhusu mada mbalimbali kwa mujibu wa ruwaza ya mtaala mpya. Uhusishaji wa shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji. Ujumuishaji wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika shughuli za ufunzaji na ujifunzaji wa Kiswahili. Ushirikishaji wa wanafunzi wenye mahitaji maalum. Ujumuishaji wa maswala mtambuko katika shughuli za ujifunzaji. Waandishi wa kitabu hiki ni walimu wenye tajriba pana katika ufundishaji wa Kiswahili katika kiwango cha shule za msingi. Kitabu hiki kimeandamana na Mwongozo wa Mwalimu wenye maelezo ya kina.

Additional information

Authors Douglas Wangira, Tom Nyambeka
Language Swahili
Publisher Storymoja
ISBN 9789966629555