Amerudi

KSh 250.00

Description

Longhorn Tamthilia – Amerudi ni mchezo wa kuigiza unaokidhi mahitaji ya mtaala wa kiumilisi kwa mwanafunzi wa Gredi ya 8. Tamthilia hii inamsisimua, inamwelimisha, inamhamasisha na kumburudisha msomaji kwa njia ya kipekee. Pendo, msichana wa Gredi ya 8 anaasi kila lililo jema. Vipindi katika runinga pamoja na mitandao ya kijamii imemvuruga akili. Babake Pendo, Bwana Ooko, hapatikani nyumbani. Ameadimika kama maziwa ya kuku katika malezi ya mwanawe. Pendo anatoroka shuleni na kisirisiri,  anafanya biashara ya  dawa za kulevya kwa kushirikiana na Nyau, mwanamke anayeuza dawa za kulevya. Pendo anasakwa na wazazi, mamlaka ya shule, polisi na marafiki. Je, ni nini kitamfanya Pendo arudi shuleni? Je, baba yake Pendo, Bwana Ooko atarudi nyumbani kumtafuta  mwanawe? Nyau aliyewatoroka polisi atarudi na kuyakiri na kuyatubu makosa yake? Amerudi ni tamthilia tatuzi, yaani ni tamthilia inayokusudia kutatua baadhi ya matatizo ya kisasa ya malezi. Utatuzi huu unafanyika kupitia kwa kuishirikisha jamii pana katika kuyaelewa matatizo ya kisasa yanayowakabili  vijana na hasa wanafunzi. Kila mmoja anafaa kujirudi na kurudi katika njia mwafaka kitabia, kimatendo na kifikira ili kupata suluhu ya changamoto za malezi. Amerudi ni mwangwi wa methali ‘Mui huwa Mwema’.

Additional information

Authors Murungi M. James, Rehema Makokha
Language Swahili
Publisher Longhorn Publishers
ISBN P9789966644275