Description
Longhorn Diwani ya Mashairi ni mkusanyiko wa mashairi ya arudhi na huru yanayohusu maisha ya binadamu katika jamii inayobadilika kwa kasi. Mashairi yaliyo katika diwani hii yanakidhi mahitaji ya mtaala wa kiumilisi kwa mwanafunzi wa Gredi ya 9. Mashairi mepesi na ya kuvutia katika diwani hii yanamulika kwa jicho pevu masuala mtambuko katika jamii kama vile: lishe bora, utunzaji wa mazingira, haki za kibinadamu, uhuru wa wanyama, usawa wa kijinsia, mshikamano wa kitaifa, utatuzi wa migogoro, matumizi ya pesa, usalama barabarani, kuheshimu tamaduni za wengine, mazoezi ya mwili, vifaa vya kidijitali na mengineyo. Ubunifu wa watunzi wa mashairi katika diwani hii unadhihirika kwa namna walivyofinyanga na kuipamba lugha ili kuwasilisha ujumbe kwa njia ya kupendeza na kusisimua. Mtindo wao wa kuwasilisha masuala mtambuko ni wa kupigiwa mfano. Diwani hii itawafaa wanafunzi, walimu na wasomaji wanaochangamkia ushairi wa Kiswahili. Watunzi wa mashairi yaliyo katika diwani hii ni walimu wenye tajiriba pana na pevu katika ufundishaji wa ushairi katika viwango mbalimbali vya elimu.