Description
�Punde alipolitupia jicho tangazo hilo, aliinua kichwa na kutazama dari kwa muda wa takribani dakika mbili hivi kabla ya kuinama na kushika magoti mfano wa mtu aliyesokotwa na tumbo. Alikiona kiza kizito kilichomfanya kuchemsha bongo. Ni tangazo ambalo lilimsafirisha mbali kuwawazia wanawe Jilani, Dilani na Zani aliowapenda si kidogo bila kumsahau mkewe Jamila na kichinjamimba wao Bani. Dhoruba ya kupoteza kazi inamwatua sana Jabali moyo. Inamfungulia milango ya masaibu ya kila nui. Maskani yao mtaani Buruburu yanageuzwa kuwa uwanja wa mafarakano yasiyokwisha baina yake na mkewe. Mmiliki wa maskani hayo nayo yamechacha akidai haki yake. Milio ya simu haikomi kusikika kutoka kwenye benki ikimkumbusha yeye ni mdaiwa. Alifanya nini kukwepa mafuriko ya masaibu haya?