Description
Matendechere anaona kwamba wazazi wake hawamthamini na kwa hivyo haamini anaweza kupata matokeo bora. Anaposoma tangazo kwenye bango shuleni kuhusu mchezo wa kuigiza unaopangiwa kufanyika katika shule yake, anaamua kujitafutia nafasi ya kushiriki ingawa ana wasiwasi. Atafanikiwa? Soma hadithi ujivumbulie!