Majabali Yanapoyeyuka

KSh 250.00

Description

�Mwanasaikolijia alirudi kumwangalia mgonjwa wake akiwa ameridhika kwa matokeo ya jitihada zake kumshawishi Subra. Akaanza kuliwazia tatizo la binadamu kujiruhusu kutawaliwa na historia. Alikubali kwamba kila mtu aliathiriwa na usuli wake, lakini aliamini kwamba lilikuwa kosa kuibeba historia ya maisha kama mzigo ambao unakuzuia kusonga mbele…” Historia inayorejelewa ni machafuko baada ya uchaguzi huko Medani kwa kina Subra.Mhasiriwa huyu alishuhudia mauji ya mumewe na kuteketezwa kwa makao yao na genge la wanamgambo likiongozwa na jirani yao Kondo, aliyegeuka kuwa adui. Yeye na watoto wake wawili wanaponea chupuchupu na kukimbilia mji mkuu. Kwa sadfa ya ajabu, familia za mhasiriwa Subra na muuaji Kondo zinaletwa pamoja tena miaka kumi na miwili baadaye. Mgogoro mkali unazuka kuhusu usuli wa familia za Subra na Kondo, haswa uadui wao wa zamani, unapobainika. Mgogoro huu uliosheheni taharuki unapata ufumbuzi mwishoni mwa hadithi. Unapoisoma mpaka mwisho, ndipo unapouvumbua.

Additional information

Authors Mwenda Mbatiah
Publisher Queenex Publishers Ltd
ISBN 9789966141477