Description
“Katika Mchezo wa Mtelezo, Mwalimu mkuu anawashauri wanafunzi kwenda nyumbani mapema kwani shule yao itatumiwa kugawa chakula cha msaada. Hata hivyo, baadhi ya wanafunzi wanakiuka ushauri huo. Wanajiingiza katika mchezo wa mtelezo kwa muda mrefu. Hawajali athari za kushindana na kutumbukia majini. Mvua kubwa inapoanza kunyesha, inawalazimu wanafunzi hao kutafuta mahala pa kujikinga. Masaibu yao yanachacha wanapojikuta mikononi mwa mwalimu mkuu. Soma hadithi ujifahamishe adhabu wanayopata.”