Mvulana Aliyeibiwa Urithi na Hadithi Nyingine

KSh 250.00

Description

Mvulana Aliyeibiwa Urithi ni hadithi inayomhusu mvulana yatima kwa jina Machozi. Machozi anapitia mateso ya kila aina akiwa katika mikono ya mlezi wake baada ya kifo cha wazazi wake. Machozi ananyanyaswa, ananyimwa haki ya kupata elimu miongoni mwa haki zingine za kimsingi. Hii ni hadithi yenye uwezo wa kumtoa msomaji machozi. Inaonesha jinsi tamaa inavyoweza kumfanya binadamu kusababisha uovu usio mfano. Tujifunze Pamoja ni msururu wa hadithi zilizoandikwa kwa kuzingatia mtalaa wa umilisi. Lengo la msururu huu ni kumwezesha mwanafunzi kupata ujuzi wa kuimarisha stadi ya kusoma, kukuza maadili yake na kumsaidia katika kufanya maamuzi ya busara maishani.

Additional information

Authors Yahya Mutuku
Publisher Queenex Publishers Ltd
ISBN 9789966141422