Description
Kijulanga alizaliwa katika mazingira magumu yasiyosikika wala kutajika. Hali hii haikuiua ndoto yake ya kufanikiwa. Tabia njema na bidii yake zilimfanya aheshimike na walimu pamoja na wenzake shuleni. Wavyele wake walipoipa dunia kisogo, ilionekana kana kwamba hataweza kuifikia ndoto aliyokuwa nayo. Mfadhili wake anauawa kwa sumu na kisha mke wa mfadhili kukatisha ufadhili. Je kijana huyu atafanyaje ili kufanikiwa maishani na kuifikia ndoto yake?