Description
Baraka na Zawadi ni watoto walio na matamanio ya kuzuru maeneo mbalimbali ulimwenguni, kununua vitu vya thamani na kuwanunulia wazazi, marafiki na walimu wao tuzo za thamani. Wanaokota kitita cha pesa, je, watafanya nini? Hadithi hii inalenga kukuza maadili ya kusema ukweli na kuwa mwaminifu.