Description
Ziara ya Meno ni hadithi ya pili katika msururu wa ‘Mazingira na Afya’. Kitabu hiki kinashughulikia usafi na afya ya meno. Lengo hili limetimizwa kupitia safari ya akina Baraka na Zawadi. Njia za kutunza na athari za kutotunza meno zimewekwa wazi kupitia majadiliano baina ya wahusika. Je, wahusika wananufaika mwisho wa kikao?